Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa hayo.
Tukio hilo
limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili, wasanii Agnes Gerald
Masogange na Melisa Edward kukamatwa kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika
Kusini wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na
thamani ya Sh6bilioni.
Aidha,
hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini
kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia katika Pwani ya
Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa za kulevya aina ya
bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50milioni (Sh125 bilioni).
Kaniki na
Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis
Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa
safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.
Kaimu
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel Shelukindo alithibitisha jana kwamba
wanamichezo hao wanashikiliwa nchini humo na Polisi wa Kitengo cha Uchunguzi wa
Makosa ya Jinai.
Wanamichezo
hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakamu Kuu ya Ethiopia iliyoko kwenye eneo
la Arada, Addis Ababa kujibu tuhuma za kubeba kilo saba za dawa hizo haramu.
Mkwanda anadaiwa kubeba kilo nne wakati Kaniki akidaiwa kubeba kilo tatu. Kama
watapatikana na hatia, wanaweza kufungwa kifungo cha miaka tisa hadi 15.
Alisema
uwezekano wa kesi ya Kaniki na Matumla kurudishwa Tanzania haupo kwa kuwa nchi
hizi mbili hazina utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
“Wameshikiliwa
hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10 sasa, sisi tulipigiwa simu na polisi wa hapa
Alhamisi iliyopita kujulishwa kwamba kuna Watanzania wawili wameshikiliwa kwa
tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya, tulipokwenda tukamkuta ni Kaniki na
Matumla,” alisema Shelukindo.
“Wao
wenyewe wanaeleza kwamba walipitia Mombasa na huo mzigo walipewa na mtu mmoja.
Lakini Kaniki yeye anajitetea kwamba huyo aliyewapa huo mzigo pale Mombasa
anajuana vizuri na Mkwanda. “Kwa hiyo alichofanya yeye ni kuubeba tu. Walikuwa
wapitie hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndipo warudi Sweden kwa njia zao wanazojua
wenyewe. Walipofika hapa Mkwanda alifanikiwa kupenya akapanda ndege lakini
Kaniki akanaswa na mbwa ndipo akajitetea kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa
lake lakini mizigo mingine ilikuwa ya Mkwanda.
“Ndipo
hapo sasa Mkwanda akashushwa kwenye ndege wakashikiliwa na Jumatatu ya wiki
iliyopita wakapandishwa kwenye Mahakama ya hapa kutajiwa kesi yao lakini
hawakupewa nafasi ya kujitetea. Kesi itatajwa tena Jumanne (leo) na Jumatano
(kesho) na uchunguzi wa polisi bado unaendelea.”
Wanamichezo
hao walidai kwamba walikabidhiwa mizigo hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mombasa
walipokuwa wakikabidhiwa pasi za kupandia ndege baada ya kupita sehemu zote za
ukaguzi.
No comments:
Post a Comment