facebook likes

Monday, September 16, 2013

MBUNGE WA MASWA MAGHARIBI JOHN SHIBUDA ASEMA SIASA SI MATUSI BALI NI KUKOSOANA KWA HOJA

1

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa CHADEMA jimbo la Maswa Magharibi Mh. John Shibuda wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Meatu mjini Meatu, 
SOMA ZAIDI....
ambapo ameelezea kuwa Siasa siyo ugonvi na alikuja Meatu kwa sababu mbili tu Moja ilikuwa ni kukutana na Ndugu Kinana kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali juu ya tatizo la zao la Pamba kuhusu bei ya zao hilo na matatizo ya pembejeo kwa wakulima wa Wilaya hiyo, Akaongeza kwamba jambo la pili ni kuwa Ndugu Abdulrahman Kinana ni rafiki yake wa muda mrefu, kwani hata wakati wakisoma shule walisoma wote Mosh,i Abdulrahman Kinana akisoma Old Moshi Sekondari na John Shibuda Mwenyewe akisoma Moshi Technical lakini pia akasema wakati alipokuwa akigombea ubunge wa Maswa Magharibi Kinana alimchangia shilingi Milioni moja "Siasa nia Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana kwa hoja" amemaliza Shibuda.

3 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo katika mkutano huo huku Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi John Shibuda akimsiliza, kushoto anayetabasam ni Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye.4 
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano huo kushoto ni John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...