07
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne (kulia) akimkabidhi Redds  Miss Tanzania Happiness Watimanywa mfano wa hundi wakati akimkabidhi msaada wa  mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) itakayojengwa mkoani Shinyanga. wa pili kushoto ni Mkuu wa Nidhamu wa Miss Tanzania, Albert Makoye na Meneja Mahusiano  ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’souza. 
SOMA ZAIDI......Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
06 (2)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige mfano wa hundi wakati akimkabidhi msaada wa  mifuko 600 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule na zahanati zitakazojengwa mkoani Shinyanga. Katikati ni  Meneja Mahusiano  ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’souza. Hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
03
Mshindi wa tatu wa Redds Miss Tanzania 2013, Clara Bayo akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Pascal Lesoinne wakati wa hafla hiyo. Katikati ni mshindi wa pili, Latifa Mohamed na kulia  ni Redds Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa. Msaada wote wa mifuko 900 ya saruji unagharimu shs milioni 30.
.Twiga Cement yakabidhi msaada wa Saruji kwa Redds Miss Tanzania 2013 kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya wenye Ulemavu wa Ngozi 
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya saruji ya Twiga (TPCC) ya jijini Dar es Salaam imetoa mifuko ya saruji 900 yenye thamani ya shilingi Milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na ujenzi wa zahanati na shule ya msingi jimbo la Msalala, wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Pascal Lesoinne alisema Twiga wana matumaini kwamba msaada huo utasaidia kusukuma mbele maendeleo ya elimu na afya nchini.
“Tunatazamia kwamba tutaendelea kuwekeza katika sekta ya afya na elimu kwa pamoja, na kama mnavyofahamu kwamba sekta hizi zina changamoto kubwa na za muda mrefu,”
“Kampuni ya Twiga kwa sasa inatazamia kujikita katika kuzumgumza kwa kina mambo ya biashara na sehemu tunazoweza kushirikiana kati ya kampuni na watu wa Shinyanga pamoja na wawakilishi wao kama wabunge ili kuweza kusaidia maendeleo ya wananchi kwa manufaa yetu zote,” alisema.
Alisema kwamba kampuni ya Twiga ipo nchini Tanzania tangu mwaka 1959 na imeonyesha mafanikio makubwa na chanya katika kutoa mchango wa kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya taifa.
Lesoinne aliongeza kwamba mifuko 300 ya saruji itatengeneza kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) baada ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika sehemu za kahama mkoa wa Shinyanga.
Alisema sehemu nyingine ya mifuko ya saruji 600 aliyokabidhiwa Mbunge wa Msalala, Mhe Ezekiel Maige itajengwa zahanati na shule ya msingi katika jimbo hilo kupunguza matatizo ya madarasa na vituo vya afya katika mji wa Shinyanga.
Kwa upande wake, Mhe Maige alishukuru kampuni ya Twiga kwa msaada wao katika jimbo lake na kusema itapunguza mzigo mkubwa kwa serikali ya mkoa na wadau wengine wa maendeleo katika sekta hizi.
“tutajenga shule ya msingi Bihangija katika jimbo la Msalala ili kuhakikisha watoto wetu wanasoma katika mazingira mazuri yatakayowawezesha kusoma na kufaulu,” alisema.
Alisema matatizo na changamoto katika sekta za afya na elimu ni kubwa na za muda mrefu zinahitaji wadau kwa pamoja kushirikiana na si kuiachia serikali peke yake.