facebook likes

Wednesday, September 11, 2013

GARI LA KUBEBEA WAGONJWA LAKAMATWA LIKITUMIKA KATIKA WIZI NDANI YA MGODI GEITA.

Mwandishi wa habari Denice Stephano anaripoti kwamba gari la kubebea wagonjwa  limekamatwa likitumika katika wizi ndani ya mgodi wa Geita na kufanya wapatikane watuhumiwa tisa wa kesi ya wizi wa mafuta katika mgodi huo wa Dhahabu ( GEITA GOLD MINE ). 
 SOMA ZAIDI....
Mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta Abiner ameiambia mahakama September 9 2013 kwamba 5/09/2013 saa 7:30 usiku huko eneo la Geita power ndani ya mgodi wa Geita gold mine watuhumiwa waliiba mafuta lita 630 ya dizeli, kula njama za kuiba mafuta hayo na kuharibu mali ambayo ni gari la kubeba wagojwa katika kituo cha Afya cha Nzera kwa kuling’oa viti...
 
Mtuhumiwa wa kwanza Hamudi Biemo (28) Dereva wa gari anatuhumiwa makosa matatu likiwemo la kula njama na kung’oa viti vya gari.
1
Abiner ameongeza kuwa washitakiwa hao walitumia gari aina ya Land Crusser yenye namba za usajili T 671 AKW mali ya Halmashauri ya wilaya ya Geita  na kuingia mgodini kuiba mafuta aina ya Diesel lita 630 yenye thamani ya Tsh. 1,386,000/= mali ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)


Waliofikishwa mahakamani ni Hamudi Biembo dereva wa gari la wagonjwa ,Malemo Paul (31)  mkazi wa mtaa wa  Mseto Geita,Selemani Magoso (31 )ambaye ni dereva pikipiki mkazi wa mtaa wa Shilabela Geita, Julias Boazi (28) mkazi wa Msalala road Geita ). Wengine ni Rashid Hussen (27) -Mlinzi wa mgodi, Ismail Zuber (26) -mlinzi wa Kampuni ya G4S ,Christoper Kombo -Operator wa GGM,Joseph Chiristopher (27) -Operator wa GGM
2
Wakili wa upande wa utetezi Leonard Bitemo baada ya watuhumiwa kusomewa mashitaka yao na kukana, aliiomba Mahakama ya wilaya kuahirisha kesi hadi wiki tatu  ili wateja wake ambao ni Selemani Magoso, Boaz Paul na Milemo Paul wapate nafasi ya kujiandaa kwa ajili ya utetezi....
 

Madai hayo yalipingwa na  mwendesha mashtaka  wa poisi na kuomba mahakama ipange  siku za karibu badala ya wiki tatu kwani kuna mashahidi ambao wanasafiri kwenda nje ya nchi, kesi hiyo itajwe 12/09/2013 ambako watakuwa wamejiandaa na
kuomba mahakama ipange  siku za karibu badala ya wiki tatu kwani kuna mashahidi ambao wanasafiri kwenda nje ya nchi, kesi hiyo itajwe 12/09/2013 ambako watakuwa wamejiandaa na mahakama ilikubaliana na uamuzi huo na washitakiwa wote (9) wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti. 3

5

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...