facebook likes

Sunday, August 18, 2013

HUYU NDO MSANII WA BONGO MOVIE AMBAYE WATU WANASEMA ANA JINSIA MBILI, SOMA HAPA ALICHOKISEMA KUKANUSHA

Zahra Mohamed
Zamo mwigizaji wa filamu Swahilihood.
MSANII na mtayarishaji wa filamu Swahilihood Zahra Chambo Mohamed aka Zamo anasema kuwa anachukizwa sana na tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimuongelea bila kujua ukweli kuhusu maisha yake halisi,
...SOMA ZAIDI.... jambo ambalo limekuwa likimkwaza hasa ni kuambiwa yeye ana jinsi mbili kitu ambacho si kweli na kwanini wamuongelee vitu hivyo?
.
Zahra Mohamed
Zamo akiwa katika pozi katika kochi.
Zahra Mohamed
Zamo akiwa katika pozi.
Zahra Mohamed
Zamo msanii wa filamu.
“Mtu anasema kuwa mimi nina jinsi mbili aliwahi kunichungulia hadi aseme hivyo, na kama kweli sasa mimi ninajisaidiaje nikiwa na jinsia mbili jamani? Watu wanapoteza muda wao kwa kunijadili mimi kuhusu jinsia yangu iwasaidie nini siku hizi kuna mambo ya utandawazi, unaweza kumuona mtu yupo hivi au vile lakini isiwe jibu sahihi kwako, jibu ni Question Mark,” anasema Zamo.
Msanii huyo amelalamika kwa kusema kuwa kuna mtangazaji mmoja wa Televisheni alimletea matatizo sana katika familia yake baada ya kuongelea vitu ambavyo yeye anasema vya kijinga kwa kushangaa jina lake kitu ambacho alisema ni tofauti na malengo, akiongea nasi mtandao mahiri wa habari za filamu Bongo anasema kuwa kuanzia sasa hatokuwa na urafiki na watu au watangazaji wanaotaka kiki kutoka kwake.
Hivi sasa Zamo anatamba na filamu yake ya Question Mark sinema anayosema inaelezea maisha yake kwa asilimia kubwa, na hata wale wenye mashaka na jinsia yake waitafute na kuiangalia kwa ajili ya maisha halisi ya Zamo na kumaliza utata kuhusu yeye ni nani?

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...