facebook likes

Monday, July 8, 2013

Wafanyakazi wa ujenzi wamdhalilisha Kim Kardashian hadharani


Kampuni moja ya ujenzi iliyopo Canada, imeamua kumtest Kim kwa kuweka bango linalochekesha na kumdhalilisha katika jengo la Bay Adelaide Center lililopo Toronto, Ontario, ambalo liko katika ujenzi
Katika lakini katika juhudi za kupunguza wasiwasi kwa umma, wajenzi wa jengo hilo waliweka bango linalosema kuwaambia wenyeji, 'Ujenzi kumalizika kwa kasi zaidi kuliko ndoa Kim Kardashian.'

, "Construction set to finish faster than a Kim Kardashian marriage."
inasemekana bango hilo lilitengenezwa na kundi la wachekeshaji ambao ni ma-legendari "Second City" ikiwa ni sehemu ya utani utakaokuwa ukiendelea mpaka pale project hiyo ya ujenzi itakapokamilika.

kama story imekuacha njia panda ni hivi, Kim Kardashian alifunga ndoa na Kris Humphrey, ambayo ilidumu kwa siku 72 tu kabla ya kuvunjika.

Ilivyokua kwenye Big Brother Africa The Chase weekend ya July 7

bba8_20130707_day42_lastwords_hakeem_fatima_lg
Hakeem na Fatima
Big brother Africa The Chase kupitia DSTV channel 197 na 198 inazidi kumiliki headlines na washiriki wanazindi kupungua kwenye jumba hilo kuelekea fainali ambapo wiki iliyopita tulishuhudua mshiriki wa Tanzania Nando kuwa kwenye dangerzone ya kutoka ndani ya jumba hilo lakini bahati nzuri ni kwamba hakutolewa hiyo July 7.
Washiriki wawili Fatima kutoka Malawi na Hakeem kutoka Zimbabwe ndiyo wamesema byebye kwenye jumba la Big brother Africa weekend iliyopita kuangushwa kwenye kura.
944705_394022090718613_841348358_n
Kura zilivyoenda wiki hii
wakazi_live_lg1_74d1aab9-1a24-4e1d-bbad-f477f8add475_101307201017067
Wakazi akiwa kazini
Kitu kingine kilichomiliki headlines kwenye Big brtoher wiki hii ni show ya msanii kutoka Tanzania Wakazi a.k.a Swaga Bovu ambaye alipiga show kali na ngoma zake mbili Weekend na Touch.

"PREZZO ANAYAJUA MAPENZI.....HATA AKINIUDHI SITAHESABU MAKOSA YAKE"....DIVA WA CLOUDS FM


Muda mfupi uliopita mtangazaji wa ‘Ala za Roho’ ya Clouds FM Diva Loveness Love ambaye sasa anatumia “divathebawse” katika akaunti yake ya Instagram, ameweka picha mpya akiwa na Rapcellency Jackson makini aka Prezzo kutoka Kenya waliyopiga jana (July 7).


Picha hiyo ambayo inawaonesha wawili hao wakiwa “0 distance” ilikuwa na caption inayosomeka hivi,

“Nothing Than Happiness… Prez is such a Nice guy. Hata Akiniudhi Sihesabu makosa yake. May you Live Long Pleaseeee……… Good hearted, My hero, My Mentor… A Person I can count to when I need to be happy… No one is Perfect yes but I love his flaws and All…. Bless you always’ . I Pray you live Long… I Pray for you Always”


Picha nyingine iliwaonesha Prezzo na Diva wakikumbatiana na kusindikizwa na caption “Last Night at escape1… I was nothing than happy. With Prezzo”.




Prezzo alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza jana (July 7) katika show ya Matumaini iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Bong5

Unajua single inayofata ya Ommy Dimpoz inaitwaje? kafanya na nani? .

.
.
Kwenye interview fupi na millardayo.com Ommy Dimpoz amesema single yake inayofata itaitwa ‘Tupogo’ ambayo amemshirikisha J Martins wa Nigeria, imefanywa na maproducer wawili ambao ni Marco Chali na Man Water wa Combination Sound.
Audio yake inatarajiwa kutoka hivi karibuni ambapo itatangulia alafu video ikishafanywa ndio itafata kwa kutoka baadae, hii itakua single ya nne ya Ommy Dimpoz kutoka baada ya ‘Nai nai’ aliyofanya na Ally Kiba, ‘baadae’  na ‘Me and you’ aliyofanya na Vanessa Mdee.

MWANAFUNZI WA CHUO CHA VETA MKOANI DODOMA AJILIPUA KWA PETROL.....KISA NI WIVU WA MAPENZI


MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na mwanafunzi huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.

Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua.

“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.

“Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).

Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.

WANAWAKE WAWILI WAMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA AFRIKA KUSINI WAKITOKEA TANZANIA


Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema wanawake wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.


Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.


“When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa.

 Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema Muller.

Wanawake hao ambao hawakutajwa majina wala uraia wameshikiliwa na polisi nchini Afrika Kusini.

Historia yatengenezwa kwenye fainali ya Wimbledon Tenis.

Mwanadada toka UFaransa Marion Baroli ameweka historia ya kuwa mwanamke wa 18 kutwaa ubingwa wa michuano ya tenis ya Wimbledon akimshinda Mjerumani Sabine Liscki .
Bartoli ambaye alishinda kwa seti mbili bila majibu akishinda kwa michezo 6-1 na 6-4 aliweka historia nyingine ya kuwa mwanamke pekee kutwaa ubingwa wa Wimbledon bila kucheza na mchezaji aliyeko kwenye top 10 ya viwango vya Ubora duniani Huku pia akiwa mchezaji wa kwanza ambaye hayuko kwenye top 10 kutwaa ubingwa katika historia ya michuano hiyo.
Sabine Licki alionekana kuzidiwa tangu mapema kiasi cha kuanza kububujikwa machozi kabla ya mchezo kuisha hali iliyomfanya apoteze mwelekeo na kupoteza mchezo huo. Mwanadada huyo ameondoka na kitita cha dola milioni 1.6 kama zawadi ya kutwaa ubingwa huo .
Fainali hiyo kwa upande wa wanaume itafanyika hapo kesho ambapo Andy Murray wa Scotland atacheza na Novak Djokovic wa Serbia .

Marion Bartoli akionyesha Taji lake.
Marion Bartoli akionyesha Taji lake.
Sabine Licki alishindwa kuzuia machozi kwenye seti ya pili.
Sabine Licki alishindwa kuzuia machozi kwenye seti ya pili.

Chek na video mpya ya Mrwanda Alpha Rwirangira na Lamyia Good

.
Lamyia Good.
Nakualika kuzitumia dakika zako 3 kutazama video mpya ya mshindi mara mbili wa Project Fame Kenya Mrwanda Alpha Rwirangira ambae this time kamshirikisha Lamlyia Good ambae ni ndugu wa tumbo moja na mwigizaji staa wa Marekani, Meagan Good…
Lamyia ndio yuleyule mrembo ambae alinogesha ile single ya ‘speak with ya’ body’ ya Ay ft Romeo Miller na Lamyia mwenyewe

Uliziona picha 10 za 50 Cent akionyesha ufahari nyumbani kwake na kusisitiza kwamba hayuko jela?

Rapper 50 hivi karibuni amekua kwenye headlines kwa kudaiwa kumfanyia fujo nyumbani kwake mpenzi wake wa zamani ambapo adhabu ya kosa hilo inaweza kuwa miaka mitano jela au kulipa faini….. sasa baada ya kuwekwa kwenye headlines sana 50 Cent amemua kutoa picha akiwa amerelax na kusisitiza kwamba hayuko jela, yuko huru tena batani.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 1450

Pata kujua maana ya tatoo yenye maandishi ya kichina aliyojichora Nicki Minaj.

minaj (2) 

Onika Tanya Maraj maarufu kama Nicki Minaj member wa Young Money ambaye amezaliwa miaka 30 iliyopita, anasifika kwa style yake ya kurap na jinsi anavyojifananisha na mdoli wa barbie. Kitu kingine ambacho Nicki Minaj anacho ni tatoo ambayo ipo kwenye mkono wa kushoto iliyoandikwa kwa lugha ya kichina. So, umewahi kujiuliza nini maana ya tatoo ile ambayo Nicki Minaj amejichora. Kama ulikuwa hujui ni kwamba hiyo ndiyo tatoo pekee ambayo Nicki Minaj anayo kwenye mwili wake tofauti na boss wake Lil Wayne ambaye karibia nusu ya mwili wake una tatoo.
Kwenye lugha ya kiingereza tatoo hile maana yake ni ”God is always with you”, kwa kiswahili ni kwamba “Mungu siku zote yupo pamoja nawe”. Sources zinasema kwamba Nicki Minaj mwenyewe anasema alijichora hiyo tatoo akiwa na akili za kitoto na kama akiweza kurudi nyuma asingeweza kuichora tena.

 

Mjue nyota wa Barcelona alie mbioni kujiunga Manchester United.

Picha mbili tofauti .
Picha mbili tofauti .
Sehemu iliyozungushiwa duara jekundu kulia inamuonyesha Thiago akiwa amevaa jezi ya Man United enzi za utoto wake.
Sehemu iliyozungushiwa duara jekundu kulia inamuonyesha Thiago akiwa amevaa jezi ya Man United enzi za utoto wake.
Namba 11 ilikuwa jezi ya Thiago sasa itavaliwa na Neymar.
Namba 11 ilikuwa jezi ya Thiago sasa itavaliwa na Neymar.
Jezi namba 11 ambayo itavaliwa na Neymar msimu ujao.
Jezi namba 11 ambayo itavaliwa na Neymar msimu ujao.
Mbio za klabu bingwa ya England Manchester Uited kumsajili nahodha wa timu ya taifa ya Hispania Under-21 Thiago Alcantarra zina uwezekano mkubwa wa kumalizika kwa mafanikio kufuatia taarifa ya mpango uliopo wa kukutana kwa viongozi wa Barcelona na Manchester United wiki ijayo.
Barca ambao awali walikuwa wazito kuzungumza na United juu ya usajili wa Mchezaji huyo kwa kuwa wanamtazama kama mrithi sahihi wa nafasi ya kiungo Xavi Hernandez  lakini kwa hatua iliyofikia hawana jinsi zaidi ya kukubali kwa kuwa tayari mchezaji mwenyewe amefanya maamuzi ya kuondoka.
Tayari makubaliano ya kimsingi baina ya Mchezaji (Thiago Alcantarra) na Manchester United yamefanyika ambapo inaaminika kuwa mchezaji huyo atasaini mkataba wa miaka mitano ndani ya United kwa thamani ya Euro milioni 18.
Barcelona wanaonekana kukata tamaa ya kubaki na mchezaji huyo kama zinavyoonyesha baadhi ya ishara ikiwemo taswira ya mchezaji huyo kuondolewa kwenye picha ya uzi duzi wa jezi mpya za klabu hiyo ya Hispania,namba ya jezi aliyokuwa anaivaa ( jezi namba 11) kupewa kwa mchezaji mwingine ambaye ni Neymar huku kukiwa na ripoti kuwa baba mzazi wa mchezaji huyo ambaye ni nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Mazinho kuuza mgahawa wa familia ulioko huko Catalunya zote hizi zikiwa ishara ya kujiandaa na maisha nje ya Hispania.
Endapo United itafanikiwa kumsajili mchezaji huyo atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa baada ya nyota wa timu ya taifa ya Uruguay Under-21 Guilermo Varela kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na David Moyes kama kocha mpya wa United.

Ligi ya Ufaransa yajiandaa ku-Make headlines kwa usajili wa mastaa kibao.

Edinson Cavanni ameripotiwa kujiunga na klabu ya PSG.
Edinson Cavanni ameripotiwa kujiunga na klabu ya PSG.
Katika miaka ya hivi karibuni nyota wengi wakubwa kwenye ulimwengu wa soka wamekuwa wakivutiwa na soka la Hispania na wengine soka la England, hali hii inatokana na ukweli kuwa ligi hizo ndio nyumbani kwa timu kubwa barani ulaya kifedha na kimafanikio na hata umaarufu pia , hali hiyo inakaribia kubadilika kufuatia kuibuka kwa klabu nyingine yenye msuli mkubwa wa kifedha nchini Ufaransa ya Monaco.
Kuibuka kwa Monaco kunafanya mbio za ubingwa wa Ufaransa kuanza mapema kwa mbio za ligi ya Ufarans

Lulu anyakua tuzo kwenye moja ya tamasha kubwa la filamu barani Africa.

lulu pic
Elizabeth Michael maarufu kwenye bongomovie kama Lulu na maarufu kwenye mitandao ya kijamii kama hotlulumichael, hivi karibuni nyota yake imeendelea kung’aa tena kwenye tamasha kubwa la filamu africa. Kupitia category ya “Best Actress Swahili Movies” ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwepo wa wasanii wengi wa kike wanaofanya vizuri kwa sasa, lakini Elizabeth Michael a.k.a Lulu amenyakuwa tuzo hii kwenye tamasha la ZIFF ambalo ni maarufu na linahudhuriwa na wadau mbalimbali wa filamu kutoka sehemu tofauti duniani. Hivyo basi hii itakuwa ni fursa nyingine na nzuri kwa Lulu baaada ya wadau wa movie kumjua yeye na labda kufuatilia kazi zake kitu ambacho kinaweza kumsaidia kufika zaidi ya hapa alipo sasa kwa kupata kazi nyingine nje ya Tanzania. Lulu ameshinda tuzo hii kutokana na ushiriki wake kwenye movie ya Woman of principle. Movie hii iliandaliwa na kampuni ya RJ Company na kufanywa na Ray,Lulu na Nagris Mohamed kama washiriki wakuu.
lulu
woman_of_principles_208_294
TRAILER YA WOMAN OF PRINCIPLE

Will Smith alitoa Summer time na mwanae Willow kaja na Summer fling

willow-smith-short-hair
Summer time ni ngoma maarufu sana ya actor na mwanamuziki Will Smith. Moja kati ya ngoma ambazo hadi leo zikiwekwa kwenye maeneo ya starehe bado watu wanazielewa kutokana na ukali wake. Hiyo ilikuwa ni miaka ya 90, lakini 2013 mwanae Will Smith ambaye ndiyo binti wa pekee kwenye familia yao akiwa na kaka zake wawili…Willow Smith na yeye ametoa ngoma ambayo inafanana kidogo jina na Summer time lakini wake unaitwa Summer Fling. Nakupa nafasi ya kuiona na video yake kwa mara ya kwanza mtu wangu wa nguvu kama bado haijakufikia.

Hii ndio ndege ya Asian Airline iliyopata ajali, imeua na wengine wamejeruhiwa.

crash

Kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha San Francisco nchini marekani kumetokea ajali ya ndege iliyohusisha ndege moja ya Asian Airline ambayo iilkuwa na abiria wengi kutoka bara la Asia ambapo mpaka ajali imetokea watu walioweza kujulikana uraia wao ni wachina 141 ambao kati yao kuna wanafunzi wa high school 32 wakitokea China kuelekea Marekani kwenye summer camp, abiria 77 ni wakorea, 61 Wamarekani, Wahindi 2 na taarifa zaidi ni kwamba watu karibu 180 wamekimbizwa hospitali baada ya kupata majeraha na waliofariki hadi sasa ni watu wawili tu. Kutokana na maelezo ya maofisa wa Asian Airline, ndege yao haijapata crash hii kutokana na tatizo la injini bali kuna tatizo lingine ambali bado halijajulikana kwa sababu hali ya hewa ilikuwa shwari kabisa, kwenye mabaki ya ndege hiyo wataalamu wameweza kupata kifaa kinaitwa black box ambacho hurekodi mambo yote ya safari ya ndege, hivyo basi itasaidia katika kupata majibu juu ya sababu ya ajali hii.
VIDEO YA JINSI ABC NEWS WALIVYO REPORT HII AJALI



Cheka kidogo hapa mtu wangu wa nguvu upate starter ya jumatatu na wiki nzima.

a.baa-Its-monday-again...

Mtu wangu wa nguvu wiki ndiyo imeshaanza na jumatatu ndiyo hii. Najua wengi monday ni siku ngumu sana hasa pale unapotafuta energy ya kurudisha hali ya kazi. Basi kama vipi nakupa vipande hivi vya vichekesho ambavyo vitakupa starter nzuri ya jumatatu yako mtu wangu wa nguvu na uendelee na kazi kama kawaida
Kimombo na sms, Jamaa katumiwa meseji na girlfriend wake. Kutokana na urefu wa meseji hiyo ikashindwa kufika yote,  mwishoni ikaandika some text missing. Jamaa kizungu hajui hivyo maneno ya mwisho hakuelewa maana yake lakini akahisi litakuwa neno la kimahaba, kujifanya aonekane mjanja akajibu.. “some text missing too dear”
………….
Kuna majambazi walifanikiwa kuingia Bank na kuiba Pesa nyiingi sana na kufanikiwa kutoroka. Wakafika sehemu wakaanza kuzihesabu hadi wakachoka kuhesabu. Mmoja akawambia, “Oyaa mi nimechoka kuhesabu tusubiri taarifa ya habari itangaze tumeiba Sh Ngapi.”
…………
Baba: Mwanangu ehe, shika hii shilingi 500 usimuambie mama yako kuwa nimelala na housegirl.
Mtoto: Sitaki, tatizo we baba ni mbahiri sana mwenzio mama akilala na dereva ananipaga shilingi 1,000
…………
WAZO LA JUMATATU
Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mshahara.
Masista doo watavaa vimini vyote lakini sio mini kabaang
…………
Mke: kuna nini kwa jirani??
Mme: kutakuwa kuna birthday..
Mke:ya nani??
Mme:itakuwa ya TUYU
Mke: TUYU ndo nan?
Mme: sijui ndo nani nimesikia wanaimba Happy birthday Tuyu,
………..
Mjukuu akamnon’goneza Babu, “Naomba mia tano”. Babu alikua hana kitu akajifanya hajasikia ninong’oneze sikio la huku hilo bovu. Mjukuu akamnong’oneza kwenye sikio lingine “Babu naomba elfu tano”. Babu akahamaki nooo huku ndio sisikii kabisaaa bora kule ulikoomba mia tano nadhani ntasikia! mjukuu hoi!.
………
Jamani uoga huu….!!!
Familia moja ilivamiwa na majambazi basi ilikua hivi.
JAMBAZI:wewe mama unaitwa nani.?
MAMA:mimi naitwa ASHA
JAMBAZI:una bahati sana jina lako kama la marehem mama yangu hivyo sikuui….,
na wewe baba unaitwa nani…?
BABA:mimi naitwa ATHUMANI lakini kazini wamezoea kuniita ASHA kama marehemu mama yako
……….
Mwalimu Alisimama Darasani Akauliza
Mtu Ambaye Mjinga Asimame…Madenge Akasimama Peke yake
Mwalimu: Wewe ndo Mjinga???..
Madenge: Nimeona nisimame Usiwepeke yako..
………
Mke alifariki dunia akakutana na mumewe mbinguni ,mke akamwambia mumewe” mume wangu bora tumekutana tuendeleze mapenzi yetu” mume akajibu tuliapa kifo ndo kitatutenganisha huku mbinguni nipo single na kuna malaika namfukuzia kwahyo usinijue!
………..
Jamaa kamdanganya girlfriend wake kuwa anasomea HOTEL MANAGEMENT.
Siku huyo girlfriend akamkuta jamaa anaosha vyombo kwa MAMA NTILIE.
Girlfriend akamuuliza jamaa “beby vipi mbona uko hapa?”
Jamaa bila woga akajibu “NIPO FIELD”.
………….
source: millardayo

Lowassa awapa milioni 20 wafanyabiashara wadogowadogo wa jijini Mwanza !

Mhe. Lowassa akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 20 Bw.Matondo ambaye ni mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa wafanyabiashara wadogowadogo wa jijini Mwanza (SHIUMA) huku akishuhudiwa na diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha (anayepiga makofi). 


Bw. Lowassa alisema kwamba kutokana na marafiki zake ambao aliwataja Bw.Christopher Mwita Gachuma (MNEC- Tarime), Bw.Mathias Manga (MNEC-Arumeru), Bw.Raphael Chegeni (MNEC-Busega) Bw.Shanif Hiran Mansoor(Mbunge-Kwimba) na Bw.Altaf Mansoor (Mkurugenzi wa MOIL) ambao waliniomba na kunisisitiza kuwaona na kuwasikiliza nami nimewapa utaratibu wa kuandaa Harambee kubwa ya kuwachangia na marafiki zangu wengine.

“Leo hii siyo harambee bali nataka kuwachangia kianzio katika mfuko wenu na siku zote CCM inasema kwamba ni lazima kuwapatia mtaji vijana hivyo nawapatia Cheki ya milioni 10 na jioni ntwapatia shilingi milioni 10 jumla zitakuwa shilingi milioni 20 za kuanzia ili kujipanga na harambee kubwa




Mmoja kati ya wanakamati wa SHIUMA akionyesha hundi ya shilingi milioni 20 waliyokabidhiwa na Mhe. Lowassa kama sehemu ya harakati ya kutatua masuala mbalimbali ya changamoto zao walizoziainisha kwenye risala.
Lowassa akiwapa somo wamachinga Mwanza.

WAZIRI Mkuu mstaafu Bw.Edward Lowassa amewataka wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwawezesha wafanyabiashara wadogo maarufu kwa MACHINGA ili kuwawezesha kupata mitaji ya kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na Machinga wa shirika la SHIUMA kwenye eneo la Makoroboi Jijini Mwanza leo mchana Mhe. Lowassa ambaye ni Mjumbe wa NEC  Wilaya ya Monduli na Mbunge wa Jimboni humo alisema njia pekee ya kuwawezesha wamachinga hao ni kuwachangia fedha ili kuwawezesha kujiendeleza kupitia biashara zao na kuwapatia maeneo maalumu ya kufanyia shughuli zao.

Maneno yaliyowagusa.
“Ninyi ni watanzania wenye kujiamini na kujitafutia ridhiki kwa kufanya biashara zenu kwewnye Taifa lenu mkiwa huru na amani, lakini mkiwa hamna mijati hamtaweza kufika pahali popote hivyo niwaombeni sana wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwachangia ili kuwawezesha kupata mtaji wa kuwaendeleza  na kujiingizia kipato katika biashara zenu za ujasiliamali”alisema.
Makoroboi jijini Mwanza.
Mjumbe huyo wa NEC alisema kwamba Ilani ya CCM inatambua na inaelekeza kwamba vijana wataandaliwa na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali (SACOS) na kusajiliwa ili kuwapatia fedha ikiwa ni mitaji ya kuwawezesha kujiendesha jambo ambalo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ukurasa wa 88 na 89 hivyo tunataitekeleza kwa vitendo kama ambavyo ninyi tayari mmeanza kuitikia na hilo ndilo limenileta hapa leo nikiwa kiongozi ndani ya CCM.

“Nitaka nirudie msimamo wangu kwenu kwani kuna baadhi ya vyombo vya habari vinaniandika kwamba nimekuja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Bw. Mwiguru Mchemba (Mbunge wa Jimbo la Iramba)kuvunja ngome ya Chama furani hapa maeneo ya Jiji la Mwanza siyo kweli mimi niko na marafiki zangu nimekuja kutokana na wito wenu ili kuwasikiliza sasa puuzeni hayo”alisema.
Mkutano huo wa muda mfupi ulipo malizika tu Mhe. lowassa akiwa ameambatana na wamachinga mguu kwa mguu walimsindikiza hadi hoteli aliyofikia. PICHA ZOTE KWA HISANI YA G-SENGO

KASEBA AINGIZA FILAMU YA BONGO MAFIA MTAANI


BINGWA wa mchezo wa Kick Boxing nchini Chapion Japhert Kaseba ameingia katika fani ya utoaji filamu za mapigano Live akianzia na picha yake ya kwanza itakayo mtambulisha inakwenda kwa jina la Bongo Mafia

Filamu hiyo iliyo rekodiwa katika ubora wa hari ya juu sasa ipo mtaani Ikisambazwa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya wapenzi wa filamu nchini wajionee vitu tofauti kidogo kwani kuna wakali kibao alio washirikisha 
Picha hiyo ni mfululizo za picha zake nyingine ambazo zipo njiani kwani amekuja kufanya kazi katika jamii  ili watambue ipi pumba na upi mchele
Bongo mafia ilioshilikisha wasanii kama vile ,Dotnata,Kelvin,Muhogo Mchungu,Pendo Njau Champion na Rogers MASTER SHIVO,na Wasanii wengine kibao

Amesema filamu hiyo kwa sasa ni gumzoo mtaani wakati ndio kwanza inamaliza wiki moja tangu kuingia sokoni 

Kaseba ambaye hivi karibuni ali mdunda bondia Rasco Simwanza wa Malawi amejitamba kuendeleza ubabe  kwa mabondia wengine huku akifanya kazi zake za sanaa ambazo kwa kiasi kikubwa anamshukuru sana Dotnata kwa kuona kipaji chake hicho ambacho kilikuwa kimejificha na sasa kipo mtaani

Kaseba amesisitiza kwa mashabiki wake wamuunge mkono kwa kununua kazi hiyo kwani ndio kwanza ananza kulishika soko la filamu hapa nchini endapo wataendelea kumunga mkono na ndipo watakapofuraia kazi zake nyingi zilizopo jikoni kwani nina kazi tofauti tofauti Nne hivi na sijui nianze na ipi ndio mana nimeamua kutoa hii kwanza alisema Kaseba.

Boy kills his girlfriend by sitting on her head















 
A man was arrested and charged with murder after sitting on his girlfriend’s head until she died, according to police reports.

A central Pennsylvania man suffocated his 17-year-old girlfriend, by sitting on her head after he intentionally drove into a guardrail at 100 mph in the middle of the night, officials said.


Police filed murder and other charges Friday against Benjamin Daniel Klinger, 19, for the death of Sammi Heller on an interstate near Manheim. Klinger is accused of crashing on purpose, then killing Heller by sitting on her until she suffocated.


"At first glance, this appeared to be just another tragic accident," Lancaster County District Attorney Craig Stedman told a local Pennsylvania newspaper. "However, the police worked hand in hand with our forensic experts who saw this was as a much more complicated and sinister criminal scheme," he added.


Based on medical records, the investigators concluded later that Klinger was pretending to be unconscious. Detectives recovered marijuana, cash, a digital scale, a pipe, pills and a black gun from the accident scene.


Klinger was also charged with aggravated assault, drug offenses and driving violations.


Several months ago Klinger faced a charge of simple assault for allegedly running over the foot of Heller and two counts of disseminating sèxually explicit material to a minor for allegedly sending photos and videos of Heller.

BBA Live Show: Tanzania’s Wakazi Kills It Off Live Show: Tanzania’s Wakazi Kills It Off



After a whole week of waiting for the young talented Tanzanian “Wakazi” to perform on the live eviction eviction show, he has finally done his thing on the Big Brother Africa stage.
He has began by performing a great jam titled “Weekend/Touch” which was a combination of both English and Kiswahili ryhmes with a lot of energy which totally left all the Big Brother Africa fans crazy and while he was putting out his rymes, all the sexy girls were tirelessly cheering the sexy Tanzanian rapper.



Later after Fatima and Hakeem had been evicted from the Big Brother house, Wakazi stepped again on the Big Brother Africa stage with another killer jam titled Sexy Lady.
He completely killed it off with this one because even the evicted Fatima could not hold it anymore, she stood and started dancing to the tune of the song.

Bolt made a brief return to the Big Brother audience in a pre-recorded interview to share his thoughts on his experiences in the House.

After that Live Show Presenter IK crossed over to the Ruby and Diamond Housemates to chat to the Chasemates.

Stay tuned to DStv channels 197 and 198 for all your Big Brother Africa The Chase action or catch the daily shows on Africa Magic Entertainment (DStv channel 150) at 20:00 CAT.

SURUALI ZA KUBANA KWA MWANAUME NI HATARI


Dk Vincent Kafuuza wa Kituo cha Friends Polyclinic & Ambulance Service alisema siyo tu kuhusu suruali za kubana, lakini nguo zozote za kubana siyo nzuri kuwa mavazi ya kila siku.
Alieleza kuwa mwili unahitaji kupumua, hali ambayo hufanyika kupitia kutoka jasho kwenye vinyweleo kwenye ngozi na jasho linatakiwa kukauka lenyewe taratibu.
Dk Kafuuza alisema ikiwa mtu amevaa jinzi ya kubana au nguo ya ndani ya kubana, jasho litagandana kwenye vinyweleo vya ngozi na wakati mwingine inaweza kusababisha
magonjwa ya ngozi kama vile ‘fangasi’, maumivu ya mwili na vipele katika mapaja na sehemu zingine za siri.
“Wanaume ambao wanavaa suruali za kubana wana hatari ya kupunguza kiwango cha mbegu za uzazi.
Na wakati mwingine zinaweza kupungua kwa kiwango kikubwa na kumfanya mwanamume ashindwe kumpa ujauzito mwanamke,” alisema Dk Kafuuza.
Dk Kafuuza alisema suruali za kubana zina kawaida ya kusukuma ndani sehemu zinazotunza mbegu za uzazi za mwanamume, hali inayosababisha matatizo kama vile uvimbe na ngozi kubabuka.
Nguo za ndani za kubana zinazuia kukuwa kwa mbegu za uzazi.

Wakati joto la kawaida la mwili ni sentigredi 37, mfuko wa mbegu za uzazi wa mwanamume unahitaji kiwango cha joto kati ya sentigredi 35.5 na 36 ili kufanya kazi katika hali ya kawaida.
Dk Charles Kiggundu ambaye ni Mshauri wa Hospitali ya Mulago na Chuo Kikuu cha Afya cha Makerere, alisema joto la mbegu za uzazi za mwanamume linaweza kuongezeka ikiwa mfuko unaozishika utafifia ndani ya mwili kwa muda mrefu, kwa mfano kama mwanamume amevaa nguo ya ndani ya kubana.
Kwa mujibu wa Dk Lawrence Kazibwe wa Hospitali ya Mulago, alisema mbegu za uzazi za mwanamume ziko kwenye mfuko maalumu kwa sababu zinahitaji kuwa zimepoa zaidi ya maeneo mengine ya mwili, ili ziwe kwenye mazingira tulivu.
Alisema lengo hilo linaweza kuvurugika iwapo mwanamume atavaa suruali ya kubana ambayo itazifanya mbegu za uzazi zikose mawasiliano ya kawaida na sehemu nyingine ya mwili, ambayo ni kupata joto linalotakiwa.
“Baadhi ya wanaume wanafikiri kusafirisha mbegu za uzazi pekee kwa mwanamke ndiko kunawezesha mwanamke kupata ujauzito, lakini urutubishaji hauwezi kutokea katika sehemu za kikeni,
kwa kuwa mbegu za uzazi lazima zipite kwenye mrija unaotakiwa kukutana na mayai mengine.
Hivyo basi mbegu za uzazi zinahitaji kuwa na nguvu na nyingi ili ziweze kuyafikia mayai ya kikeni na kuwezesha kupata ujauzito,” alifafanua Kiggundu.
Kiggundu alisema; “Hebu fikiria katika hali ambayo mbegu za uzazi ni chache na dhaifu! Hii ina maana hazitaweza kurutubisha mayai ya kike.
Hivyo unaweza kutoa mbegu za uzazi wakati wa tendo la ndoa, lakini hakuna ubebaji mimba utakaofanyika.”
Mbegu za uzazi ambazo ni dhaifu, kama vile zile ambazo hazina mkia, zenye mkia mkubwa, zenye mkia mdogo, zilizopinda kichwani na zile zenye mikia miwili, haziwezi kupenye kwenye mrija wa kwenda kwenye mayai ya uzazi ya kike.

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...