AJALI MBAYA KATI YA GARI NA BODABODA YATOKEA ASUBUHI YA LEO HUKO MKOANI MARA....TUNAOMBA RADHI KWA KUZIONYESHA PICHA ZA TUKIO...!!
Ajali
mbaya imetokea asubuhi ya leo majira ya saa 2 kwenye barabara ya majita
karibu na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina ya VX land cruser namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya mjini musoma kuelekea kamnyonge.
SOMA NA ANGALIA PICHA ZAIDI....
Kamera
yetu imemshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa ni abiria akiwa
anavuja damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda mchache
askari wa kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na
kumchukua kwa ajili ya kumuwahisha hospitali. Mashuhuda
walioshuhudia ajali hiyo kabla ya camera ya blog hii kufika eneo la
tukio muda mchache wamesema dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kupakia
abilia alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali
iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.