HAWA NDIO WABUNGE WATANO WANAOCHANGIA SANA BUNGENI NA WASIOCHANGIA
Uchambuzi
umeonyesha kwamba Wabunge wanaotoka katika vyama vidogovidogo na vyenye
viti vichache huwa na wastani wa juu zaidi wa ushiriki. Tathamini hii
inazingatia ushiriki uliofanywa na Wabunge katika miaka miwili ya
kipindi cha ubunge cha 2010 – 2015. Wabunge wanaweza kushiriki kwa namna tatu: kwa kuuliza maswali ya msingi, maswali ya
nyongeza
na kutoa michango. Katika namna zote hizi, TLP ambacho kina mbunge
mmoja na NCCR-MAGEUZI watano, , vilikuwa na kiwango kikubwa zaidi chaa
ushiriki kwa Mbunge. Hata hivyo, ukiondoa vyama vidogovidogo vyenye
chini ya asilimia 5 ya uwakilishi Bungeni, Chadema kinafanya vema zaidi,
kikifuatiwa na CUF na CCM.
No comments:
Post a Comment