SERIKALI YA UGANDA YAJIPANGA KUWANUNULIA WABUNGE WAKE TOLEO IPYA LA IPAD ILI KUPUNGUZA GHARAMA ZA STESHENARI
Chama cha Forum for
Democratic Change (FDC) kimepokea na kukubali mpango wa serikali ya
Uganda wa kununua toleo jipya kabisa la iPads kwa ajili ya wabunge,
lakini kimesema wabunge hao wakopeshwe na sio wapewe bure. Msemaji wa Chama hicho Wafula
Oguttu ambae pia ni mbunge, amesema pendekezo la kununua iPads
halikataliwi lakini hakuna sababu ya kuwapa bure na badala yake wapewe
kwa mkopo. Serikali ya Uganda imepanga kununua iPads za kisasa na kuwapatia wabunge kwa lengo la kupunguza gharama ya steshenari. Uamuzi huo ulichukuliwa hivi karibuni na Kamati ya Bunge na unasubiri utekelezaji kwa Kamati ya Mikataba.
No comments:
Post a Comment